Kiongozi wa Waislamu wa Dhehebu la Ismaili Duniani Mtukufu Aga Khan leo amehitimisha ziara yake ya Siku Mbili  Nchini kwa Mwaliko wa Rais John Magufuli ambapo ameagwa na Waziri wa Ulinzi Hussein Mwinyi kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Mwalimu Julius Nyerere.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Paul Makonda ni miongoni mwa Viongozi waliomsindikiza Mtukufu Aga Khan ambapo amesema ujio wa Kiongozi huyo umekuwa fursa kubwa kwa Taifa katika nyanja mbalimbali ikiwemo Afya, Elimu, Uchumi na sekta nyingine.

Amesema kuwa Uwekezaji mkubwa uliofanywa na Mtukufu Aga Khan kwenye Hospital, Shule na Hotel umekuwa na Tija kwa Taifa katika kutoa fursa za Ajira.

Hata hivyo, wakati Mtukufu Aga Khan anaondoka Uwanja wa Ndege alimuuliza Makonda kitu gani anataka afanyiwe kwenye Mkoa wake ndipo Makonda akamuelezea Kampeni ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu.

Ambapo Aga Khan amepokea kwa asilimia mia moja na kutoa maelekezo kwa wasaidizi wake nchini kumuunga mkono ambapo wameahidi kukabidhi mchango wao kwenye ofisi ya mkuu wa Mkoa hivi karibuni.

Amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya inayopelekea Viongozi wakubwa ulimwenguni kuja Nchini mara kwa mara.

Itakumbukwa kuwa hata kwenye kampeni ya upimaji wa Afya bure moja ya Hospital zilizojitolea kumuunga mkono ni pamoja na Aga Khan.

Jafo azitaka halmashauri kurejesha fedha
Ni zamu ya waamuzi daraja I na II

Comments

comments