Serikali mkoani Tabora imesitisha likizo kwa muda kwa Maafisa Ugani  na Watumishi wote wanaowatakiwa kuwasaidia wakulima ili waweze kulima kilimo kinachozingatia utalaamu kwa ajili ya kuwawezesha kuzalisha mazao mengi na kwa tija.

Hayo yamesemwa na mkuu wa mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri wakati akifunga kikao kazi cha siku tatu cha Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi Watendaji, Wakuu wa Idara  na Vitengo na Sekretarieti ya Mkoa huo.

Amesema kuwa wakati msimu wa mvua unakaribia kuanza sio vyema watumishi wa kada hiyo wakaanza likizo kwani wanapaswa kutumia kipindi hicho kuwafanya kazi ya kuwasaidia na kuwaelimisha wakulima ili wafanye vizuri katika shughuli zao na kuleta maendeleo kwa mkoa na Taifa kupitia mavuno mazuri watakayopata.

Aidha Mkuu wa Mkoa wa Tabora amewaagiza Maafisa Ugani wote kuondoka maofisini na kwenda kwa wakulima katika kipindi hiki ili kuhakikisha kila mkulima anazingatia kanuni bora za kilimo kulingana na mazao anayolima.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Igunga John Mwaipopo aliunga mkono hatua ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora ya kusisitisha likizo za Maafisa ugani na kusema kuwa Maafisa hao kazi zinapendeza wakati wa msimu wa kilimo na sio wakati mwingine.

 

Video: Sitafuta Mwenge kamwe katika uongozi wangu- JPM
Video: Itazame 'Penthouse Floor' ya John Legend akiwa na Chance the Rapper