Agizo la Rais Dkt. John Magufuli la kutaka Baraza la Madiwani la Jiji la Dar es salaam likutane kuamua matumizi ya fedha zilizolipwa kununua hisa za Shirika la Usafiri Dar es Salaam (Uda), limesababisha makada wawili wa Chadema kugombana kikaoni.
Kampuni ya Udart, inayoendesha mradi wa mabasi yaendayo kasi, ililipa Sh5.8 bilioni kukamilisha ununuzi wa hisa za Uda na hivyo Rais kuamua madiwani wakutane kujadili matumizi yake.

Aidha, upande mmoja ulitaka baraza la madiwani lisipitishe uamuzi wa kutumia fedha hizo kwa madai kuwa mchakato wa uuzaji wa hisa hizo kwa Udart, inayoendesha mradi wa mabasi yaendayo kasi, haukufuata sheria na taratibu, wakati upande mwingine ukitaka zitumike.

Wajumbe hao wa Chadema, Boniface Jacob, ambaye ni Meya wa Ubungo na Patrick Assenga (Diwani, Tabata) walishikana mashati kwenye kikao cha pembeni cha madiwani wa Chadema kilichofanyika baada ya mkutano wa Baraza la Madiwani.
Madiwani hao wa Chadema walienda ofisi ya Meya wa Jiji, Isaya Mwita kuzungumzia suala hilo na katika mazungumzo walipishana kauli kutokana na kile kilichoonekana ni kutosimamia msimamo wa chama wa kutokubali fedha hizo zitumike kwa kuwa wanaamini mchakato wa kuuzwa kwa hisa hizo haukufuata sheria na taratibu zinazotakiwa

Prof. Maghembe avurugana na madiwani Ngorongoro
Video: RC Njombe aagizwa kuwashughulikia waliotafuna sh. bilioni 1 za ushirika