Mkoa wa Njombe umeanza rasmi kutumia kituo kipya cha mabasi mjini Njombe ikiwa ni baada ya agizo la Rais alilotoa April 10 akiwa mkoani humo kuwa kituo hicho kianze kazi baada ya siku therathini.

Ujenzi wa kituo hicho unaofadhiliwa na benki ya dunia ulioanza 2013 umekuwa ukisuasua kwa kipindi kirefu licha ya uwepo wa fedha jambo ambalo lilimkasirisha Rais Magufuli na kuamua kutoa siku therathini kwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Njombe kukamilisha ujenzi huo.

Emmanuel George ambaye ni katibu tawala wilaya ya Njombe yenye Halmashauri tatu ikiwemo mji Njombe, akizungumza mara baada ya kuanza Kutumika Kwa kituo hicho mapema alfajiri amesema serikali imefanya jitihada za lazima kukamilisha mradi huo ambao umeanza kutumika licha ya kuwepo kwa baadhi ya maeneo machache ambayo hayaja kamilika huku akitaja faida zake kiuchumi.

“Licha ya kuanza kwake kuna changamoto ndogo ndogo ambazo tunaendelea nazo na leo ndio imeanza kufanya kazi, ni stendi kubwa na ya kisasa na itakuwa ni chachu ya kwenye mapato ya halmashauri, vitu ambavyo havijakamilika ni vichache kwasababu ya mvua,amesema George

Baadhi ya madereva na abiria akiwemo Michael Msilu na Amosy Kusalula wakizungumzia kituo hicho wamepongeza hatua zilizochukuliwa na serikali huku wakidai bado kuna changamoto ya miundombinu muhimu ikiwemo jengo la abiria na eneo la mama Lishe ambayo bado yanaendelea kujengwa.

Ujenzi wa kituo hicho Kipya Cha Mabasi Mjini Njombe umegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 9 za kitanzania Ikiwa Kila Mtu anayeingia ndani ya Kituo Hicho Anapaswa Kulipa Ushuru wa Shilingi 200 na Baada ya Mabasi Kutoka Ndani ya Stendi Hiyo Kituo Cha Kwanza Kwa Barabara ya Kwenda Makambako Kitakuwa Kibena Huku Wanaokwenda Songea Kikiwa Nundu.

Mbunge Mavunde ashiriki Ujenzi wa Zahanati atoa mifuko 100 ya Saruji
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Mei 12, 2019