Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewatembelea majeruhi wa ajali ya treni katika hospitali ya rufaa ya Jiji la Dodoma.

Samia amefika hospitali hapo majira ya asubuhi ambapo ametoa maagizo kwa uongozi wa mkoa kuhakikisha wanasaidiwa kufika makwao mara watakapopata nafuu.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuzunguka katika wodi zote walikolazwa majeruhi hao na kuzungumza nao 

“Nawaagiza uongozi wa Mkoa, Wizara ya afya na Shirika la reli mshirikiane kuona wagonjwa hawa wanapata huduma zote na itakapothibitika wanaweza kuruhusiwa, wasaidieni wafike makwao salama,” Amesema Makamu wa Rais.

Hata hivyo Samia ameridhishwa na hali zao pamoja na huduma wanayopata wagonjwa hao.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 4, 2021.
Biashara zitakazo toa huduma kwa siku 30