Serikali ya Uganda, imesisitiza kuwa haiko tayari kukubali vitendo vichafu vya mahusiano ya mapenzi ya watu wa jinsia moja na kwamba, hata mashinikizo ya madola ya Magharibi hayawezi kulifanya taifa hilo lisalimu amri.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari Dkt. Chris Baryomunsi wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema Serikali ya Uganda haipo tayari kukubali vitendo vichafu vya mahusiano ya mapenzi ya watu wa jinsia moja na kwamba, hata mashinikizo ya madola ya Magharibi hayawezi kulifanya taifa hilo lisalimu amri.

Aamesema, Rais atasaini mswada huo na kuonya jamii ya kimataifa dhidi ya kile alichokitaja kama kuwatisha viongozi wa Uganda kwamba watawekewa vikwazo, huku wanasheria wa Uganda wamepitisha sheria ya hukumu ya kifo kwa watakaopatikakana na hatia ya mahusiano maovu ya jinsia moja.

Waziri wa Habari Uganda Dkt. Chris Baryomunsi. Picha ya Daily Monitor.

“Tunatunga sheria kwa ajili ya raia wa Uganda na wala sio wzungu. Kama wanataka, basi watuwekee vikwazo,” amesema Baryomunsi.

Juma lilopita Bunge la Uganda lilipitisha sheria inayoharamisha kujitambulisha kama mtu wa uhusiano wa jinsia moja au LGBTQ na kuzipa mamlaka madaraka makubwa katika kukabiliana na raia wa nchi hiyo wanaojihusiha na uovu huo.

Bunge la Uganda

Rais Yoweri Museveni amekuwa mstari wa mbele kulaani vikali mahusiano ya jinsia moja kwa muda mrefu na mwaka 2013 alitia saini sheria ya kukabilkiana na uovu huo.

Wananchi waliowengi Uganda wanasema inahitajika kuwaadhibu wanaojishughulisha na harakati za kuhamasisha uhusiano wa jinsia moja, ambazo zinatishia maadili ya kitamaduni na kidini katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Simba SC kuifuata Raja Casablanca kwa mfungu
Wawekezaji wa Kusini watua nchini, Wizara ya Madini yawapa neno