Tume ya Madini imeagizwa kuanza kutoa vibali vyote vya madini kwa wafanyabiashara wa madini katika eneo la Mahenge Ulanga ili kuondoa usumbufu wa kusafiri umbali mrefu wa zaidi ya kilomita 300 hadi mkoani Morogoro kwa ajili ya kufunga mizigo yao.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Madini Doto Biteko wakati wa ufunguzi wa tamasha la kuhamasisha fursa za uwekezaji linalofanyika katika Wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro.

Waziri Biteko amesema kuwa agizo hilo lianze kutekelezwa Novemba Mosi, 2021 ili wafanyabiashara wa madini wapate huduma zote muhimu kuanzia kufanyiwa uthaminishaji, upimaji, ukataji, ufungaji na uongezwaji wa thamani ili manufaa hayo yabaki kwa wananchi wa Ulanga.

Aidha, Biteko amesema, mchakato wa kuanzisha Mkoa wa Kimadini wa Mahenge Ulanga unaendelea ili kurahisisha shughuli za uchimbaji wa madini kwa wanachi wa Mahenge kwa kuwasogezea huduma karibu.

Biteko arahisisha biashara ya madini Ulanga
Nilivyolazimisha Nyota na Kuambulia maumivu