Agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa limeanza kutekelezwa na baadhi ya makampuni yanayozalisha makaa ya mawe hapa nchini la kuongeza uzalishaji.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya kuzalisha makaa ya mawe nchini Tancoal Energy Limited, James Shedd amesema kuwa kampuni hiyo kwa sasa inazalisha kiasi kikubwa  makaa ya mawe ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani tani 60,000 kwa mwezi.

“Kampuni yetu imeongeza uzalishaji wa makaa ya mawe kwa zaidi ya asilimia 100 na tayari magari yatumikayo katika ubebaji na uchimbaji wa makaa ya mawe yako njiani kufika huku katika eneo la mgodi ili kuzidi kuongeza uzalishaji na hatimaye tani za uzalishaji wa madini haya zitazidi kuongezeka”, alisema Bw. Shedd.

 

Hata hivyo, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitoa agizo la kuongeza uzalishaji katika mgodi huo Januari 6, 2017 mara baada ya kupokea taarifa na kutembelea katika mgodi wa Ngaka kujionea shughuli za uzalishaji katika eneo hilo.

 

Mgodi wa Ngaka uko Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma na unamilikiwa na kampuni ya TANCOAL kwa ubia baina ya NDC na kampuni ya Intra Energy Corporation ya Australia.

NI Manchester United Na Ajax Amsterdam Fainali Europa League
?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Mei 12, 2017