Huenda jana ilikua siku mbaya kwa mlinda mlango kutoka Jamuhuri ya Czech na klabu ya Arsenal, Petr Cech ambaye alionekana akiteseka kwa kukubali kufungwa mabao manne dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Emirates.

Cech ambaye alisajiliwa na Arsenal mwanzoni mwa msimu uliopita akitokea Arsenal alioneakana ni mwenye majonzi mara baada ya mchezo huo kumalizika, lakini hali hiyo ilimvagaa zaidi pale alipojikuta akiibamiza gari yeke aina ya Audi A7 yenye thamani ni Pauni elfu 65 katika nguzo za sehemu ya maegesho ya uwanja wa Emirates.

Mlinda mlango huyo aliibamiza gari yake sehemu ya mbele upande wa kushoto, alipokua akijaribu kutoka sehemu ya maegesho ya magari ya wachezaji iliopo chini ya uwanja wa Emirates.

Jambo hilo lilimtia simanzi Cech, lakini alikua hana budi kuendelea na safari yake baada ya wachezaji wote wa Arsenal kuruhusiwa na meneja wao Arsene Wenger kuondoka uwanjani hapo, baada ya kupewa mawaidha na tathmini ya mchezo.

Wekundu Wa Msimbazi Kuingia Darasani
Arsene Wenger: Tulikosa Wachezaji Wenye Uzoefu