Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero amerejea mazoezini ikiwa ni siku 11 tangu alipopata ajali ya ya gari na kuvunjika ubavu mjini Amsterdam.

Klabu ya Manchester City imesema mshambuliaji huyo wa Argentina ataendelea kuimarisha hali yake ya mwili ili kurejea kikosini baada ya kuanza kufanya mazoezi mepesi hapo jana.

Aguero  mwenye umri wa miaka 29 anahitaji bao moja pekee kufikia rekodi ya ufungaji mabao katka klabu ya Manchester City aliyoiweka Eric Brook ambayo ni mabao 177.

City wanaongoza katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza kwa wingi wa mabao, mbele ya Manchester United, na watakutana na Stoke siku ya Jumamosi.

Sergio Aguero alipata ajali baada ya teksi aliyopanda kugonga boriti ya taa barabarani mjini Amsterd Uholanzi alikokwenda kuhudhuria onesho la mwanamuziki wa Colombia Maluma.

Mtuhumiwa hatari wa uhalifu auwawa
Juan Antonio Pizzi akubali lawama, kujiweka pembeni

Comments

comments