Mwanamke mmoja aliyetajwa kwa jina la Ally Opfer, mkaazi wa Ohio nchini Marekani amekuwa mmoja kati ya wanawake wanaosherehekea siku ya leo kwa kushuhudia miujiza iliyomtokea.

Opfer ambaye alifikishwa hospitalini na kufanyiwa uchunguzi na madaktari wa awali ambao walidai kuwa alikuwa na tatizo la mchanga kuingia kwenye figo, aligundulika kuwa ana ujauzito nusu saa kabla ya kuhamishiwa kwenye chumba cha kujifungulia.

Akielezea hali yake kabla ya kufikia hatua ya kujifungua, alisema kuwa aliendelea kupata hedhi kama kawaida kwa miezi mingi na kwamba hata ilipokoma alijua ni hali ya kawaida ya mabadiliko ya mwili.

Amesema kuwa kabla ya tukio hilo ambalo lilimkuta Disemba mwaka juzi, alikuwa akifanya vipimo hospitalini lakini mara kadhaa vipimo vilionesha kuwa hakuwa na ujauzito.

“Nilikuwa najisikia vizuri, sikuwa nimeanza kuonesha, kila kitu kilikuwa katika hali ya kawaida. Labda kwa sababu ya namna ambavyo nilikuwa nimembeba wakati mtoto wangu wa kiume alikuwa tumboni. Kwakweli hata sielewi ni kwanini sikuwa naonesha,” Opfer anakaririwa na The Insider.

Kutokana na matatizo ya uzazi, madaktari walimsaidia kujifungua kwa njia ya upasuaji siku moja kabla ya usiku wa kuamkia Krismas (Disemba 23) na akamuita mwanae Oliver ambaye hadi leo ana afya nzuri.

Ahmed Abdulraof awapa matumaini Simba SC
Kesi ya watuhumiwa wa bomba la mafuta yapigwa danadana