Mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa amewaomba wananchi kumpa ridhaa ya kuwa rais ili aigeuze Tanzania kuwa ‘nchi ya maziwa na asali’.

Ahadi hiyo inatoa picha ya nchi yenye maisha bora na yenye furaha kama ilivyokuwa ahadi waliyopewa wana wa Israel wakati wakiwa katika utumwa nchini Misri, kuwa wanatakiwa kumsikiliza Nabii Musa ili awafikishe kwenye nchi ya maziwa na asali ambayo ni ‘Kanaani’, kwa mujibu wa Biblia.

Lowassa aliyasema hayo katika mkutano wake wa kampeni hivi karibuni mjini Singida ambapo aliahidi kuipaisha nchi kimaendeleo.

“Nipeni fimbo niwaletee maendeleo katika nchi hii. Nia yangu ni kuiona Tanzania ikiwa moja kati ya nchi kubwa kiuchumi barani Afrika. Kwa kutumia rasirimali nyingi tulizonazo majirani zetu watatuona tukiwa mbali sana,” alisema.

Pia Lowassa aliwaahidi wakulima na wafugaji wanapata pembejeo na mahitaji ili wafanye ufugaji wa kisasa utakaowanufaisha zaidi.

“Nilichaguliwa, serikali yangu itatoa pembejeo zote muhimu na motisha katika kilimo mbali na kuwaruhusu wakulima kuuza mazao yao kokote wanakotaka,” aliongeza.

 

 

Waisrael Wafikisha Ujumbe Kwa Njia Ya Soka
Utafiti: Nani Mshindi Urais 2015?