Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli ameahidi kufanya kazi kwa ukaribu mkubwa na Rais wa Zanzibar kulinda amani ambapo amesema atampa ushirikiano wa kutosha kukamilisha aliyoahidi

Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo leo Novemba 13, 2020, wakati akihutubia na kufungua bunge la 12, kwenye ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.

“Nitashirikiana na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi kulinda amani, hatutokuwa na utani hata kidogo na mtu atakayetaka kuvuruga amani na kuingilia uhuru wetu, na namuahidi Rais Dkt. Mwinyi nitampa ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha aliyoyaahidi”, amesema Dkt. Magufuli

”Katika miaka mitano hii serikali ninayoiongoza itafungua milango ya majadiliano na sekta binafsi na wafanyabishara wote ili kujadili namna ya kuondoa migogoro ya biashara ili tutengeneza mabilionea wengi wakiwemo wabunge”, amesema Dkt. Magufuli

Aidha amesisitiza kuwa serikali yake itaendelea kuboresha mazingira kwa wananchi kuongeza kipato chao ikiwemo mazingira wezeshi ya biashara.

Rais Magufuli afungua rasmi Bunge la 12
Umoja wa Ulaya wataka wabunge walioachishwa kazi Hong Kong kurejeshwa katika nafasi zao