Mwenyekiti wa  Yanga Yusuph Manji anatarajiwa kukabidhiwa rasmi timu ya yanga, baada ya mchuano mkali dhidi ya yanga na simba utaofanyika oktoba mosi mwaka huu. Ahaidi kuleta faida ndani ya miaka kumi ya utawala wake na kuchukua asilimia 75 ya mapato, huku asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.

Ahaidi kubeba hasara yoyote itayojitokeza katika timu na kusema nembo za klabu zote zitakua chini yake.

Bodi ya Wadhamini ya Yanga chini ya Fatuma Karume na Francis Kifukwe imeridhia kumkodisha rasmi Manji timu hiyo kwa miaka 10 kama alivyoomba kupitia mkutano wa dharura wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika Juni 11 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee Dar es Salaam.

Video: Imalize wiki kwa shangwe na mix ya video kali iliyopikwa na DJ Jors Bless
Mkuu wa Upelelezi Kinondoni ahukumiwa kunyongwa, Zombe na wengine wapenya