Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally amejitokeza hadharani na kumpigia Kampeni Mgombea nafasi ya Makamu wa Rais wa Young Africans Suma Mwaitenda.

Mwaitenda amejitosa kuwania nafasi hiyo, ikiwa ni mara yake ya pili kuingia kwenye Uchaguzi Mkuu wa Young Africans, akifanya hivyo miaka minne iliyopita kwa kugombea nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji.

Ahmed Ally amempigia Kampeni Mgombea huyo kwa kuwataka Wanachama wa Young Africans kumuamini, kama Simba SC ilivyomuamini Mwanamke Barbara Gonzalez kwa kumpa nafasi ya Afisa Mtendaji Mkuu ‘CEO’.

Ahmed ametumia ukurasa wake wa Instagram kuandika ujumbe wa kumpigia kampeni Suma Mwaitenda ambaye amedai ni Rafiki yake wa karibu.

Ameandika: Baada ya @bvrbvra kuaminiwa na kupewa majukumu makubwa ndani ya SIMBA hakuna aliyeamini kama angeweza na hatimae leo hii Simba tuna vuna matunda yake

Wapo Wanawake wachache wenye uthubutu wa kuongoza vilabu vikubwa

Rafiki yangu binafsi @sumamwaitenda anahitaji ridhaa kubwa ya kuwa makamu wa Rais ni nafasi kubwaa mnoo lakini sina mashaka na ubora wake na uwezo wake

Kila la @sumamwaitenda kwa maslahi ya mpira wa miguuu 👏👏

TCRA yataka weledi kwa 'Bloggers & Youtubers'
Wafungwa 600 watoroka gerezani