Wakati Klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara zikiendelea kufanya usajili wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa 2022/23, Uongozi wa Simba SC umewataka Mashabiki na Wanachama wake kuwa na subra.

Simba SC imekua kimya tangu ilipomtangaza Mshambuliaji Moses Phiri mwezi uliopita, huku wapinznai wao Young Africans wakiendelea kutambusha usajili wa wachezaji wa Kimataifa.

Meneja wa Habari na Mawasilino wa Simba SC Ahmed Ally ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwatualiza Wanasimba, kwa kuwaambia tayari klabu hiyo imeshakamilisha sehemu ya usajili wake na wakati wowote wataanza kuwatangaza wachezaji waliomwaga wino Msimbazi.

Ahmed anaandika: ‘Najua unajiuliza maswali mengi kuhusu usajili wa timu yetu 🦁🦁

Niwatoe hofu wana SIMBA wenzangu tumekamilisha sajili kadhaa za viwango vya CAF

Usajili wetu unaenda kitalaamu sana kwa sababu wachezaji tunaowachukua sio wale waliotemwa na klabu zao

Punde si punde tunaanza kuweka hadharani wachezaji wetu na utambulisho wa wachezaji wetu tutaufanya mchana kweupe sio usiku wa manane kama tunakula daku!!

‘SEMAJI ASIYEGOMBANA NA WAKUBWA’

Jemedari Said akoleza vita na Haji Manara
Abdul Sopu atambulishwa rasmi Azam FC