Uongozi wa Simba SC umesema ilikua umuache Kiungo kutoka nchini Uganda Thadeo Lwanga wakati wa Dirisha Dogo la Usajili, lililofungwa Januari 15.

Lwanga ambaye ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Simba SC, kwa muda sasa amekua nje ya Uwanja akijiuguza, na imethibitishwa huenda akarejea mwishoni mwa msimu huu.

Akizungumza kwenye kipindi cha Sports Arena cha Wasafi FM leo Jumatano (Januari 19), Meneja wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Simba SC Ahmed Alli amesema: “Thadeo Lwanga ilikuwa tusitishe mkataba wake mwezi huu kutokana na jeraha lake kuchelewa kupona na tulikuwa tayari kutafuta mbadala wake ila daktari ametuhakikishia atakuwa amepona kufikia mwisho wa mwezi huu (January)”

Wakati Huo huo Ahmed Ally amesema Mshambuliaji Kibu Dennis yupo vizuri na hakuumia sana wakati wa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbeya city, uliomalizika kwa Simba SC kukubalia kufungwa bao 1-0.

Ahmed amesema Mshambuliaji huyo yupo vizuri na leo Jumatano (Januari 19) amekua sehemu ya mazoezi sambamba na wachezaji wenzake kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mtibwa Sugar utakaochezwa Jumamosi (Januari 22) Uwanja wa Manungu Complex, Mkoani Morogoro.

Simba SC kuifuata Mtibwa Sugar kesho
Kocha Gabon atoa ufafanuzi