Meneja wa Habari na Mawasilino wa Klabu ya Simba SC Ahmed Ally amewashukia baadhi ya Mashabiki wanaomtupia lawama Kocha Msaidizi Selema Matola kwa kutaka aondolewe kwenye nafasi hiyo.

Baadhi ya Mashabiki wa Simba SC wamekua wakilaumu maamuzi ya Uongozi wa Klabu hiyo kushindwa kumuondoa Matola kila unapomfukuza Kocha Mkuu, kwa madai amekua akifanya hujuma kupitia wachezaji.

Ahmed Ally amesema lawama anazotupiwa Kocha Matola hazina maana katika kipindi hiki na badala yake anapaswa kuchukuliwa kwama mtendaji mzuri katika Benchi la Ufundi kama ilivyo kwa watendaji wengine.

Amesema lawama za kutaka Kocha huyo mzawa kuondolewa katika majukumu yake, hasa Simba SC inapopoteza mchezo dhidi ya Young Africans, ni kutokufahamu vizuri matokeo ya mchezo wa soka kwa Mashabiki ambao wamekua wakitumia hiyo kama sababu.

“Hizo lawama unazozisikia kuhusu Matola na kocha Zoran zimetokana na hakuna anayeamini kama tumefungwa. Huu ndiyo mpira unaweza usifanye makosa na ukaadhibiwa.”

“Hakukuwa na makosa ya mtu yeyote yule . Kuendelea kumtafuta mchawi hakutusaidii kwa sasa Jumatano tuna mechi muhimu ya ligi. Muda huu tujkijikite katika mechi ya Jumatano.”

“Mashabiki wanapaswa kujua safari hii tuna timu nzuri sana, Yes Yanga wana timu nzuri, lakini hawana timu nzuri ya kutuzidi sisi” amesema Ahmed Ally

Simba SC itaanza Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2022/23 kesho Jumatano (Agosti 17) kwa kucheza nyumbani Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam dhidi ya Geita Gold FC.

Kenya: Mwili wa Afisa IEBC aliyetoweka wapatikata bondeni
TFF yafanya mbadiliko Ngao ya Jamii