Mahakama nchini Marekani imemuhukumu adhabu ya kifo mzungu mwenye msimamo mkali, ambaye aliwaua waumini tisa weusi katika kanisa moja, Carolina ya Kusini.

Dylann Roof amekutwa na hatia hiyo mwezi uliopita kwa zaidi ya mashtaka 30, ikiwemo uhalifu wa chuki.

Aidha, Katika utetezi wake wa mwisho kwenye mahakam hiyo, Roof  hakuonesha kujutia makosa yake aliyoyafanya na kusema bado anahisi alipaswa kufanya mauaji hayo ya waumini wa hao weusi.

Mwezi Juni 2015, alikwenda katika kanisa moja la watu wenye asili ya Afrika mjini Charleston na kufyatua risasi wakati ibaada hiyo ikiendelea.

Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa kuhusiana na masuala ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani na kumlazimu Rais Barack Obama kutaka kumalizwa kwa ghasia zinazosababishwa na matumizi ya bunduki.

Video: Watu 12 wafa ajali ya jahazi, Mtatiro, Lipumba waingia vita mpya...
Askofu Mokiwa agoma kuachia uaskofu