Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba imemuhukumu kunyongwa hadi kufa Melchedes Burchard (30) mkazi wa Kiluluma mkoani Kagera kwa kukutwa na hatia ya kumuua kikatili mtoto wake mwenye umri wa miaka 2 na nusu kwa kumkata mapanga.

Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Lucia Kairo ambapo amesema vitendo vya mauaji vinavyoendelea kushika kasi mkoni Kagera kwa watoto ambao hawana hatia kuwa vinahatarisha usalama na amani.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo wakili wa serikali Haruna Shomari amesema kuwa ameridhishwa na hukumu iliyotolewa na mahakama kwa kuwa itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia ambazo sio za kibinadamu.

Melchedes alifanya mauaji hayo ya kikatili ya mtoto huyo Julai 27, 2015, ambapo alificcha mwili wa mtoto huyo kwenye kichaka kilichopo karibu na nyumba yake na alipomaliza kufanya hivyo alirudi na kuendelea na shughuli zake.

Kumekucha: Membe achukua fomu kugombea urais
Msumbiji yakana kuhusika mripuko wa Lebanon