Mkazi mmoja wa Kijiji cha Bahi Wiaya ya Bahi Mkoani Dododma , John Masao amehukumiwa miaka mitatu jela au kulipa faini ya shilingi milioni tano, baada ya kupatikana kwa kosa la kutuma ujumbe wa uchochezi na kulikashifu Jeshi la Polisi kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook.

Hukumu hiyo imetoleawa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, James Karayemaha ambapo imesema kuwa, Masao alitenda kosa hilo kinyume cha sheria namba nne ya makosa ya mtandao ya mwaka 2015, na anahukumiwa kifungo cha miaka mitatu kwenda jela au kulipa faini hiyo.

Aidha, akisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo namba 177 ya jinai ya mwaka 2016, Wakili wa Serikali, Lina Magoma amedai kuwa Masao alitenda kosa hilo Agosti 30, mwaka huu kupitia akaunti yake ya Facebook ambapo alituma ujumbe uliokuwa ukilikashifu jeshi la polisi.

“Hizo ni mbwembwe tu, ujue jinsi polisi yetu haioni mbele, sasa siku hiyo mkianza kupiga raia, wake zenu na watoto zenu watakuwa wanachungwa na nani? kubwa kuliko jioni mnarudisha bunduki mnakuja mtaani, kwanini msisokotwe, mwambieni bosi wenu kama mnataka mchezo na raia awajengee makambi mtoke mtaani kwetu la sivyo itwaletea mikosi”ulisomeka ujumbe wa Masao.

Hata hivyo baada ya kusomwa shitaka hilo mshitakiwa alishindwa kulipa faini hiyo na kupelekwa jela miaka mitatu, huku hakimu Karayemaha akisema rufani ipo wazi kwa pande zote mbili.

 

Azam FC Kujipima Na Mtibwa Sugar
Mugabe, Museveni kuhudhuria desemba 9