Katika hali ambayo wengi hawakuitegemea, mtu mmoja ameiba tuzo aliyokabidhiwa mshindi wa tuzo za Oscar kama muigizaji bora wa kike, Frances McDormand kwenye hafla iliyofanyika wikendi baada ya usiku wa utoaji wa tuzo hizo nchini Marekani.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mashuhuda pamoja na jeshi la polisi, mtu huyo alikwapua tuzo hiyo ukumbini na kutimua mbio, hali iliyowafanya wana usalama kumkimbiza wakisaidiana na polisi.

McDonarmand mwenye umri wa miaka 60 anadaiwa kutoka nje ya ukumbi na kuangua kilio ingawa alisikika akisema, “muacheni aende.”

Aidha, polisi wa Los Angeles jana walithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kumkamata mhusika.

“Tunaweza kuthibitisha kuwa tukio hilo la wizi lilitokea katika hafla hiyo. Tumemkamata mtu mmoja anayefahamika kama Terry Bryant kwa tuhuma za wizi,” msemaji wa jeshi la polisi wa Los Angeles aliliambia shirika la habarila AFP.

McDormand alishinda tuzo hiyo kutokana na uhusika wake kama mama anayetafuta haki ya binti yake aliyeuawa, kwenye filamu ya Three Billboards Outside Ebbing, Missouri iliyotayarishwa na Martin McDonangh.

Marekani yaingilia kati mzozo wa kisiasa wa Ethiopia
Wafuasi wa Mugabe waanzisha chama kipya, Mugabe akibariki