Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) limesema litapunguza miruko ya ndege zake sambamba na kufuta baadhi ya safari ili kutoa muda wa matengenezo ya injini.

Kwa mujibu wa taarifa ya ATCL iliyotolewa hii leo Novemba 10, 2022, imeeleza mabadiliko hayo yatatokana na changamoto za kiufundi duniani kote, ya injini aina ya PW1524G-3 zinazotumika kwenye ndege aina ya Airbus A220-300.

“Kwa kuzingatia matakwa ya usalama, tumekuwa tukifuata maelekezo ya kitaalamu ili kutoa huduma bora nay a usalama. Na wakati mwingine tunazitoa ndege katika mzunguko kukidhi matakwa ya watengenezaji wa injini hizi,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)

Taarifa hiyo imeendelea kufafanua kuwa, “Ili kuhakikisha ndege zetu zinafanya kazi kufuatana na ratiba, tutapunguza miruko na kupunguza baadhi ya safari zetu kulingana na idadi ya ndege zilizopo. Uamuzi huu ni wa muda mfupi ili kutoa muda kwa watengenezaji wa injini hizo kushughulikia matatizo yaliyopo,”.

Ihefu FC kukabili Simba SC bila Kibaya
Ugumu wa Maisha: Vijana wafikiria upya kupata watoto