Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania kwa kushirikiana na GSMA wameandaa mashindano ya suluhu za mfumo wa malipo ya pesa kupitia simu za mkononi ambayo yanafanyika jijini Dar es Salaam kwa mwaka wa pili mfululizo.

Mashindano hayo ambayo yamedhaminiwa na Airtel money na Comviva wakishirikiana na muungano wa mashirika ya simu za mkononi ulimwenguni GSMA yanajumuisha washiriki kutoka Africa. Wajasiriamali wa TEKNOHAMA kutoka Ghana, Kenya, Uganda na Tanzania watachuana kutengeneza suluhu kwenye maeneo makuu matatu, yaani malipo kwenye sekta ya usafirishaji, mfumo wa malipo ya jumla (bulk payment )na mfumo wa malipo ya pochi ya Comviva na Airtel yaani ( Airtel Comviva mobile wallet).

Aidha, Tanzania imepata fursa ya kuandaa mashindano hayo kwasababu inajulikana kama kiongozi katika sekta ya simu za mkononi inayoongoza katika kujenga mifumo ya malipo ya simu ( mobile money payment) Hivyo ni fursa ya kipekee kwa wajisiriamali wa kitanzania kuweza kutengeneza suluhu za mifumo ya malipo ya simu za mkononi zitakazotumika barani Africa.

“Sisi Airtel Tanzania tumekuwa msitari wa mbele kuwezesha wajasiriamali kwa njia mbali mbali. Kwa kupitia mashindano tunaendeleza uwezeshaji huo kwani kwa kila suluhu itakayopatikana haitaishia hapa mbali itaendelea kuboresha na kuwekwa kwenye mfumo wa malipo ya simu za mkononi,” amesema Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Isack Nchunda.

Kwa upande wake, Mkuu wa kitengo cha Teknohama GSMA, Gareth Pateman amesema kuwa washiriki wa mashindano hayo wanaweza kutengeneza suluhu moja au mbili katika zile tatu huku mshindi akipata tiketi ya kwenda Barcelona, Spain huku akiwa amelipiwa gharama zote.

Mtoto wa Jay Z achanika ndani ya 4:44, Msikilize hapa
TRA yajibu tetesi za kukagua risiti za mafuta kwa wenye magari barabarani