Airtel Tanzania imetoa msaada wa simu kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambazo zitatumika kwa ajili ya kurahisisha na kuimarisha mawasiliano ya namba ya dharura wakati wa kutoa taarifa za moto na majanga mbalimbali nchini.

Simu hizo zimetolewa kwa Mikoa yote ya Jeshi la Zimamoto ambapo wateja wa Airtel watapiga bure ilikupata huduma za Jeshi hilo.

Akikabidhi simu hizo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano amesema kuwa wao kama wanatambua umuhimu wa Jeshi hilo na wanaamini kuwa wananchi sasa wataweza kupata huduma za Jeshi hilo kwa urahisi kupitia namba hiyo ya dharura.

“Tunatambua umuhimu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika jamii, hivyo tunaamini utoaji wa taarifa za majanga kwa wakati muafaka unarahisisha shughuli za uokoaji na kuzuia kwa kiwango kikubwa cha hasara ambayo inaweza kusababishwa na majanga hayo katika jamii,” amesema Singano.

DK. Mwakyembe anena Kilimanjaro stars ikisafiri
Nawashauri Kilimanjaro Stars waisusie Libya- Zitto