Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imetangaza ofa wakati wote wa maonyesho ya biashara ya sabasaba mwaka huu zitakazowawezesha wateja wake na wale  wapya kuunganishwa na huduma za mtandao kwa gharama nafuu na pia kujipatia simu bomba kwa bei nafuu.

Katika maonyesho hayo ya biashara ya kimataifa ambayo hufanyika kila mwaka katika Viwanja vya Maonyesho ya Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Airtel imeamua kuonyesha dhamira yake hiyo ya kuendelea kuunganisha jamii kwa bidhaa na huduma bora.

Akiongea na waandishi wa habari Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando katika banda la Airtel lililopo viwanja vya sabasaba jijini Dar es salaam amesema kuwa “dhamira yetu Airtel ni kuendelea kuunganisha jamii kwa bidhaa na huduma, hivyo kwa msimu huu maonesho ya saba saba tutatoa ofa nyingi sana ikiwemo  simu aina ya ZTE GS 500, Motorola C113, Motorola F3 na Motorola C117 kwa shilingi 16,000 tu na  mteja akishanunua ataunganishwa na bando la shilingi 10,000 litakalodumu kwa muda wa mwezi mmoja” amesema Mmbando

Amesema katika kipindi chote cha sabasaba, wananchi watapata simu kwa gharama nafuu na kisha kuunganishwa na kifurushi cha mwezi mzima bure kuongea na ndugu, jamaa, na marafiki huku wakifaidi huduma zingine za Airtel.

Huduma zitakazopatikana ni pamoja na  kubadilisha laini, huduma za Airtel Money, simu za smartphone za kisasa na origino, huduma ya Timiza Vicoba, kuelekezwa jinsi yakusoma masomo ya ufundi kwa njia ya simu VETA kupitia Vsomo pamoja na kujua jinsi yakufungua biashara ya Duka la Airtel popote na jinsi ya kupata faida yako

“Airtel imekuwa ni desturi yetu kuleta huduma na bidhaa zetu katika maonyesho haya ya biashara kila mwaka na kukutana na wateja wetu ana kwa ana ili kutoa elimu zaidi kuhusu huduma zetu mpya na za kibunifu tunazozitoa kila mwaka”.

Mmbando ametoa wito kwa watanzania kutembelea banda la Airtel na kujipatia simu, huduma za kimtandao zote kwa  gharama nafuu na vilevile kukutana na watoa huduma na kupata elimu juu ya huduma mbalimbali  ikiwemo kupata maelekezo ya kupata mikopo ya vikundi kupitia huduma ya Timiza vikoba.

CCM yamng’ang’ania Lowassa, mwenyewe akomaa na yake
?LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Juni 30, 2017