Kipa Aishi Manula tayari ameshawasili nchini Afrika Kusini na kujiunga na wenzake waliopo kambini.

Manula amewasili leo Jumanne baadaya kumaliza mkataba wa kuitumikia Azam FC licha ya kuwa awali wenzake wa Simba walishaanza mazoezi kujiandaa kwa ajili ya msimu unaofuata wa 2017/18.

Pichani ni Manula akiwa na Mratibu wa timu ya Simba, Abbas Suleiman mara baada ya kuwasili na kisha kukabidhiwa jezi ya Simba.

Uchaguzi Mkuu TAFCA Agosti 10, 2017
Video: Kampeni ya Rais Magufuli ya kumtua mama ndoo yazidi kuwa neema