Meneja wa klabu ya Middlesbrough iliyorejea ligi kuu ya soka nchini England, Aitor Karanka amependekeza kusajiliwa kwa mshambuliaji wa mabingwa wa Europa League Sevilla CF, Fernando Llorente.

Karanka amependekeza jina la Llorente katika orodha ya usajili, kwa kuamini mshambuliaji huyo atakidhi haja ya kikosi chake kupambana vilivyo kwenye mshike mshike wa ligi ya nchini England, na kufikia hatua nzuri inayokusudiwa.

Mshambuliaji huyo ambaye aliwahi kuwatumikia mabingwa wa soka nchini Italia Juventus pamoja na klabu ya Athletic Bilbao ya Hispania alionyesha umahiri mkubwa msimu wa 2015-16, na kufikia hatua ya kutwaa ubingwa wa Europa League.

Hata hivyo tayari kuna taarifa za klabu nyingine mbili ambazo hazijatajwa majina kuwa kwenye mpango wa kumfukuzia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31.

Karanka amepewa jukumu la kukisuka upya kikosi cha Middlesbrough baada ya kufanikisha safari ya mapambano ya ligi daraja la kwanza, ambapo walimaliza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Chris Brown afyatuka baada ya shabiki kumshtaki kwa wizi wa ‘Kofia’
Slaven Bilic Ajitosa Kwa Carlos Bacca

Comments

comments