Katika hali ya kushangaza, madaktari wamebaini kuwa mwanamke mmoja jijini Hanoi nchini Vietnam aliyejifungua watoto mapacha, alipewa ujauzito wa mapacha hao na wanaume wawili kwa nyakati tofauti.

Kwa mujibu wa CNN, familia ya mapacha hao ilianza kuwatilia shaka kutokana na kutofanana kwao kwa kiwango kikubwa kama watoto wa familia mbili tofauti, ndipo hali hiyo ya saitofahamu na msukumo kutoka kwa baadhi yao ikawalazimu kuwaona wataalam wa afya ya uzazi.

Wataalam hao waliwafanyia vipimo vya vina saba (DNA) na jin kisha kubaini kuwa watoto hao hawakuwa wa baba mmoja.

Rais wa ‘Genetic Association of Vietnam’, Profesa Le Dinh Luong ambaye aliongoza jopo la madaktari kufanya utafiti kuhusu sakata hilo alibainisha kuwa familia hiyo ilishikwa na mshtuko baada ya kupewa majibu ya uchunguzi huo unaoonesha kuwa watoto hao hawakuwa wa baba mmoja.

Akizungumzia uzoefu wa kitabibu na utaalam kuhusu suala hilo, Dinh Luong alisema kuwa hali hiyo inawezekana ingawa ni nadra sana kutokea, hususan pale ambapo mayai ya mwanamke anaeweza kutunga mapacha yatakapokuwa yamefikia katika hali ya kuanguliwa na kisha akashiriki mapenzi na wanaume wawili tofauti ndani ya muda mfupi.

“Inawezekana kuwa binti huyo alikuwa katika siku ambayo mayai yake yalikuwa yameiva kwa kawaida mwanamke akiwa hapo anashikwa na uchu kwa sababu mwili wake unatoa mayai na unataka mwanamume atakaye mpa shahawa,” alisema Profesa Luong.

“Kwa sasa tunaamini kuwa bibi huyo alilala na wanaume wawili tofauti katika siku hiyo hiyo ambapo mayai yake yalikuwa tayari na hivyo akatungwa mimba na wanaume wawili. Hili linaweza kutokea ila ni tukio nadra sana,” alifafanua.

Hata hivyo, tukio hilo sio la kwanza kuripotiwa. Mwaka jana Mahakama ya New Jersey nchini Marekani ilimtaka mwanaume mmoja kumhudumia mmoja kati ya watoto mapacha baada ya ripoti za uchunguzi wa vina saba kubaini kuwa mtoto mwingine sio wa kwake.

 

Dk. Shein amtembelea Maalim Seif
Majina ya Wahanga wa ajali mbaya ya Daladala na Roli Dar, waliofariki na walionusurika