Kwa nchi za Afrika itakuwa ajabu kusikia mbuzi amekamatwa na jeshi la polisi na kutupwa selo kama binadamu akisubiri kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili. Lakini hii ni kawaida nchini India.

Mbuzi mmoja amepewa dhamana baada ya kukamatwa na polisi kwa kosa la kuvamia bustani ya mbogamboga ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya na kula maua na mboga aina ya ‘kabeji’.

Kwa mujibu wa Daily Mail, mbuzi huyo pamoja na mmiliki wake, Abdul Hasan,  waliweza kupata dhamana baada ya kukaa usiku mmoja lupango. Kulingana na sheria za nchi hiyo, kutokana na kosa walilolifanya, mbuzi huyo na mmiliki wake wanaweza kutumikia kifungo cha kati ya miaka miwili na miaka saba jela pamoja na kulipa faini endapo wakipatikana na hatia.

 

Mmiliki wa mbuzi huyo, Abdul Hassan,  aliiambia NDTV kuwa mbuzi wake alikamatwa na kutiwa korokoroni na alipoenda kumfuata na yeye akaingizwa ndani.

Mmiliki wa Mbuzi, Abdul Hassan

Mmiliki wa Mbuzi, Abdul Hassan

 

“Mbuzi wangu alivuka mpaka na kula maua na mboga za majani kwenye bustani. Alipelekwa katika kituo cha polisi na baadae polisi waliniingiza mimi pia,” alisema Hassan.

Chanzo: Daily Mail

 

Makampuni 210 yatumbuliwa jipu Bandarini, orodha iko hapa
Magufuli afanya tena ziara ya kushtukiza Muhimbili, akuta wagonjwa wakilala chini