Watu saba wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya kutokea ajali iliyohusisha gari kugonga na Mkokoteni uliokuwa unavutwa na Ng’ombe katika Kijiji cha Lugala kilichopo Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno amethibitisha kutokea ajali hiyo iliyohusisha gari ya Serikali Toyota Land criser na Mkokoteni uliokuwa ukivutwa na Ng’ombe hii leo Julai 3, 2022 na kusema majeruhi wote wamelekekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Diwani wa kata ya Manzase Wilayani CHamwino, John Mika akizungumza kuhusu ajali hiyo amesema gari hiyo ya Serikali iligonga mkokoteni uliokuwa umebeba watu 12 waliokuwa wakielekea katika eneo la kuchimba udongo kwa ajili ya kutengenezea vyungu.

Baadhi ya mashuhuda wakiwa katika eneo la tukio kuangalia ajali iliyohusisha Gari la Serikali kugonga Mkokoteni uliokuwa ukivutwa na Ng’ombe

“Walikuwa wanakwenda kwenye mlima wa Lugala kwa ajili ya kuchimba udongo wanaotumia kufinyanga vyungu ndipo gari hilo likawagonga, watu sita walifariki hapohapo na ng’ombe wawili waliokuwa wakivuta mkokoteni pia walikufa,” amefafanua Mika.

Mika amesema tayari majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma General kwa ajili ya matibabu zaidi.

Papa azitaka DRC na Sudan kufungua ukurasa mpya
Rasmi Waziri aifikisha tuzo kwa Rais mstaafu