Watu wanne wakimemo wawili wa familia moja wamefariki dunia papo hapo baada ya kupata ajali mbaya ya gari aina ya Isuzu walilokuwa wakisafiria mara baada ya gari hiyo kuacha njia na kwenda kugonga gema katika eneo la Kikelelwa wilayani Rombo.

Waliofariki ni Emmanuel Josephat Silayo (28), Viviano Silayo (35), wakazi wa Mbomai Juu, Juma Idd (20), maarufu kama mwarabu na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Deolla.

Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah amefika katika eneo la tukio na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kwamba dereva wa Lori hilo lililokuwa limebeba mbao alikimbia kusikojulikana baada ya ajali.

“Jitihada za kumtafuta dereva zinafanyika na chanzo cha ajali ni kupoteza muelekeo wa lori hilo na baadaye kugonga gema ndipo watu waliokuwa wamekaa mbele walichomoka na kwenda kupigiza vichwa kwenye gema na kupasuka” alisema Kamanda Issah.

Kamanda Issah amesema gari hilo likiwa na shehena ya mbao lilikuwa likitokea eneo la West Kilimanjaro, eneo maarufu wa uchanaji wa mbao na kwamba lilikuwa likielekea Rombo kupitia njia ya Rongai.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Rombo kwa ajili ya maandalizi ya mazishi.

fb_img_15366479237350140-jpg.862719

fb_img_15366479318547197-jpg.862720

fb_img_15366479388347152-jpg.862721

Mbaroni kwa kuweka video mtandaoni akilishwa na mwanamke
Mkuu wa shirika la habari ajiuzulu kwa kashfa ya ngono