Takriban Watu saba wamefariki dunia huku na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la abiria la Sheraton walilokuwa wakisafiria, kupata ajali mtaa wa Mwilima uliopo kata ya Kanyara Mkoani Geita.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi wa Polisi, Berthaneema Mlay amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema, ilihusisha basi hilo lenye namba za usajili T922 ADC iliyokuwa ikitokea Jijini Mwanza kuelekea Lunzewe, Wilaya ya Bukombe.

Amesema, ajali hiyo imetokea Machi 7, 2023 majira ya saa 10:30 jioni na kuongeza kuwa chanzo chake kilitokana na kupasuka kwa tairi la mbele kisha likachomoka na kupelekea basi hilo kwenda kuangukia mtaroni.

Kufuatia ajali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela alifika Hospital ya Rufaa kuwajulia hali majeruhi, ambapo ameliagiza kwa Jeshi la Polisi kufanya ukaguzi mara kwa mara kabla na baada ya safari za Magari ya abiria.

Wanaompinga Rais Katiba mpya wanampima: BAWACHA
Milton Karisa anaitaka Ligi ya Bongo