Jumla ya Wahamiaji 58, akiwemo na mtoto mchanga, wamekufa maji na wengine kadhaa kunusurika baada ya Boti waliyokuwa wakisafiria kuvunjika na kuzama kufuatia machafuko ya Bahari nchini Italia.

Boti hiyo, ilizama wakati ikijaribu kuweka nanga karibu na mji wa pwani wa Crotone, uliopo katika eneo la Calabria huku ikiwa imebeba takriban watu 150 wanaosadikika kuvuka Bahari kukimbia migogoro na umaskini toka Afrika hadi nchini humo kutafuta hifadhi.

Mabaki ya Boti hiyo iliyopata ajali pwani ya kusini mwa Italy. Picha ya Giuseppe Pipita/AP.

Bado haijajulikana Boti hiyo ilikuwa ikitokea wapi ingawa vyombo vya Habari nchini humo vinaripoti kuwa waliokuwemo humo walikuwa raia kutoka mataifa ya Iran, Iraq, Syria, Afghanistan, Pakistan na Somalia.

Aidha, ripoti zinasema kuwa chombo hicho pia kilizama baada ya kugonga miamba kutokana na hali mbaya ya hewa, na tayari mamlaka za Serikali nchini Italia zimeanzisha operesheni kubwa ya utafutaji na uokoaji ardhini na baharini.

Uchaguzi Nigeria: Utata waanza kuibuka
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Februari 27, 2023