Zaidi abiria 100, wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama kwenye Mto Lulonga uliopo Basankusu mkoa wa Equateur wakati wakielekea eneo la Lilanga, nchini Congo-Brazzaville.

Mbali na vifo hivyo, pia manusura wa ajali hiyo wamedai kupoteza bidhaa zote zikiwemo za chakula na wanyama huku wakisema hakuna operesheni ya uokoaji iliyofanyika ya kutafuta miili na watu waliotoweka.

Usafiri wa maji ukihusisha wafanyabiashara na ubebaji wa mizigo. Picha ya Congo Digital.

Mkuu wa shirika la kiraia mjini Basankusu, Jean-Pierre Wangela amesema “msafara wa boti ulikuwa ukielekea Lilanga na Boti hizo zilikuwa zimebeba watu wengi na bidhaa zao sasa karibu na usiku wa manane ajali hii ya boti ilitokea na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha, zaidi au chini ya watu mia mbili.

Inakadiriwa kuwa, karibu watu 145 hadi 150 walikufa majina sababu za kuzama kwa Boti hiyo inatajwa kuwa ni kupakia mzigo kupita kiasi na hivyo maji kuanza kuingia ndani hali iliyopelekea kutokea kwa tukio hilo la kuhuzunisha.

Waziri afariki ghafla akiwa kwenye kikao
Anayedaiwa kuchakachua mbolea afungiwa Leseni