Idara ya Usalama wa Umma ya Texas Marekani imethibitisha kutokea kwa ajali ya ndege iliyokuwa imebeba takribani watu ishirini na moja (21) ambao kwa bahati nzuri wote wamefanikiwa kutoka wakiwa salama licha ya ndege hiyo kuteketea kwa moto muda mfupi baada ya ajali hiyo.

Inaelezwa kuwa ndege hiyo ilikuwa inaruka kutoka uwanja wa ndege wa Houston kwenda Boston Texas nchini Marekani,eneo la karibu na barabara za Morton na Cardiff, ambapo sio mbali sana na Uwanja huo, kona ya kusini mashariki mwa Kaunti ya Waller.

Maafisa wa DPS wamesema watu 21 waliokuwa ndani ya ndege hiyo wote walifanikiwa kutoka salama isipokuwa Mtu mmoja alipelekwa hospitali akiwa na amejeruhiwa katika sehemu ya mgongoni.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 20, 2021
Ni kweli Shatta Wale amefariki Dunia?