Watu watano wakiwemo wanawake wanne na mwanaume mmoja ambaye ni dereva wamefariki dunia baada ya basi dogo aina ya hiace lenye namba za usajili T 962 BSE kugongana uso kwa uso na basi kubwa la New Force lenye namba za usajili T 346 DLY katika eneo la Lungemba -Rombo barabara kuu ya Morogoro- Iringa.

Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani mkoani Morogoro, Boniface Mbao amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa Hiace, Jackson Adam ambaye ni miongoni mwa waliofariki dunia, ambapo alikuwa akiendesha gari hiyo kwa mwendo kasi na kutaka kujaribu kilipita gari kubwa aina ya lori lililokuwa limebeba mchanga bila kuchukua tahadhari yeyote na kujikuta akikutana uso kwa uso na gari hilo la New Force.

Kamanda Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulirich Matei ametaja majina ya wengine waliofariki kuwa ni; Georgina Aloyce, Revocatus Lyimo, Mangasa Almas, na Witness Leornad ambaye ameacha watoto wawili ambao ni majeruhi katika ajali hiyo.

Ajali hiyo imetokea wakati basi la New Force likuwa linatokea Msamvu kwenda Mikese na gari dogo aina ya Hiace likiwa linatokea Msamvu, mkoani Mogororo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, amesema mbali na watu hao watano kufariki dunia, wengine tisa wamejeruhiwa na tayari wapo hospitali ya Morogoro kwa matibabu.

Aidha siku chache zilizopita kulisambaa video iliyoonesha magari makubwa mawili yakishindana na kuhatarisha maisha ya abiria, Hivyo kwa dhamana aliyopewa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba kufuatia video hiyo alitumia ukurasa wake wa twitter kuandika haya.

”Madereva wa gari yoyote (Kubwa au ndogo), kumbukeni mbeba dhamana ya maisha ya watu mliowabeba kwenye magari au wanaotembea kwa miguu, Yeyote anayehatarisha maisha ya watu wetu hatutamwacha mbali na mikono ya sheria”.

Kufuatia ujumbe huo madereva mawili wa mabasi hayo waliokuwa wakishindana walitiwa mikononi mbaroni na kufungiwa leseni zao za udereva.

Mungu azipumzishe kwa amani roho hizo tano na nyingine zilizo aga dunia duniani wakapate kupumzika kwa amani.

Pole za dhati ziwaendee ndugu, jamaa, marafiki na Taifa kwa ujumla kwa kuwapoteza ndugu zetu.

Msajili awalima Chadema barua nyingine
Kamati ya Bunge yataka kumhoji Mugabe kuhusu matrilioni