Habari zilizotufikia hivi punde ni kuwa basi (Toyota Hiace T207 CTS) la Shule ya King David Mkoani Mtwara, limepata ajali eneo la mji mwema Mikindani, na kuuwa watoto 8, dereva pamoja na msaidizi wa basi hilo huku wengine wakiwa mahututi.

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo amesema basi hilo lilifeli breki katika mteremko na kuanguka mtaroni.

Kamanda wa Polisi Mtwara Nicodemus Katembo “Wanafunzi waliofariki ni wanane, Dereva mmoja na Mwangalizi mmoja, majeruhi ni 19“

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa wafiwa, Mkuu wa mkoa na ndugu na Jamaa wote kupitia mitandao yake ya Kijamii.

Taarifa zaidi kuhusu tukio hilo endelea kufuatilia Dar 24

Raia wavamia kambi, Wanajeshi wajeruhiwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 26, 2022