Pambano masumbwi kati ya’ lililofanyika Jumamosi iliyopita katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Slaam, na kushuhudia Cheka akitangazwa mshindi wa Taji la mabara la WBF limepingwa na mpinzani wake.

Cheka alishinda pambano hilo gumu la mizunguko 12, kwa points za ushindi aliopewa na majaji watatu. Jaji namba moja, Sakwe Mtulya alimpa Cheka point 115 – 112, Jaji Anthony Rutha alimpa points 116 – 111 huku jaji namba tatu akitoa points 115-112, uamuzi uliompa nguvu muamuzi wa pambano hilo kutoka Afrika Kusini, Eddie Marshall kumtangaza Cheka kuwa mshindi.

Akiongea baada ya pambano hilo, mpinzani wa Cheka alieleza kuwa anaamini yeye ndiye aliyestahili kushinda shindano hilo na sio vinginevyo huku akidai kuwa uzalendo ndio uliombeba mpinzani wake.

“Mimi nilistahili kushinda… lakini siwezi kupingana na uamuzi wa majaji. Bado sijaamini kama nimepigwa na Cheka na niko tayari kurudiana naye,” alisema Ajetovic.

Naye Francis Cheka alimuelezea bondia huyo kuwa yuko imara na kwamba hakumshinda kirahisi.

“Nimeshinda lakini ni kwa mbinde. Mpinzania wangu alikuwa mbishi amenipa wakati mgumu kweli. Sikutarajia upinzani huu lakini nashukuru nimeshinda,” alisema Cheka.

Pambano hilo limetengeneza maoni ‘mgongano’ kwa wadau wa pambano hilo huku wengi wakimpongeza Cheka kwa kuwa imara licha ya kushambuliwa na kunusurika kushindwa kwa KO katika raundi 5 za mwanzo kutokana na mashambulizi ya mpinzani wake.

Cheka aliutumia vizuri mzunguko wa nane na kuendelea akizisaka points dhidi ya mashambulizi ya mpinzani wake, kitendo kilichomsaidia kukusanya points za kumshinda Ajetovic.

 

Video Mpya: Harmonize Feat. Diamond - Bado
Polisi wamsaka Mbunge mwingine wa Chadema, ni baada ya kuwashikilia Mdee na Kubenea