Raia wa Marekani Jocelyn Wildenstein maarufu Catwomen amefanya upasuaji wa sura mara 24 akijaribu kutengeneza uso wake ufanane na wa paka, alifanya yote hayo kujaribu kumfurahisha mumewe bilionea Alec Wildenstein aliyekuwa na mapenzi mkubwa kwa paka.

Kwa kumaungalia usoni Jocelyn amebadilika na muonekano wa sura yake haupo kama binadamu wa kawaida hali hiyo ndiyo iliyomfanya ajulikane kama Catwomen.

Pmoja na kufanya uamuzi huo wa hatari mwaka 1999 ndoa yao ilivunjika rasmi na Alec akaoa mwananmke mwingine.

Mbali na hilo yapo mambo mengi ya hatari yanayofanywa na watu waliopo kwenye mahusiano kwaajili ya kuwafurahisjha wenza wao.

Watu wengi wanjiongeza makalio, wananjichubua, wanakunywa dawa za kupunguza mwili na hata kuchora tattoo, na hapa ndipo bvijana wengi wanpoangukia kwa sasa.

Mtaalamu wa Mahusiano Deogratius Sukambi amesema vitendo vya aina hiyo ni uraibu wa mapenzi, ambapo amesema kuwa aina hiyo ya uraibu haina utofauti na uraibu wa madawa ya kulevya.

Utafiti anonyesha kuwa mwitiko wa ubongo unavyokuwa kwa mtu anayetumia dawa za kulevyana mtu amabye yupo kwenye hisia kali za mapenzi ni sawa.

”Sasa suala linalokuja hapo ni uwezo wa mtu binafsi kujitawala kihisia ili asijikute amefanya mambo ambayo yanweza kumgharimu baadaye”

Sukambi ameeleza kuwa watu wananfanya mambo mengi ya ajabu kufurahisha wenza wao kwa gharama ya kujiumiza wenyewe.

Silinde: Natoa miezi miwili daraja lianze kujengwa
Tozo za simu, miamala bado moto