Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa amethibitisha kutokea kwa vifo viwili vya wakazi wa mkoa huo ambapo mmoja ameripotiwa kuuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kichwani na kiganja cha mkono wa kulia, mwingine ameripotiwa kujiua kwa kujinyonga kisa madeni ya kikundi chake cha vikoba.

Marehemu Nuru Mlanzi yeye ni mfanyabiashara mdogo na mkazi wa Mashujaa, Manispaa ya Songea yeye amekutwa amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya manira ndani ya chumba chake alichokuwa analala.

Baada ya uchunguzi wa kina kufanyika ilibainika kwamba marehemu Malinzi aliamua kuchukua uamuzi huo wa kujingonga hadi kufa kufuatia msongo mkubwa wa mawazo uliotokanna na madeni mengi yaliyokuwa yanamkabili ambayo inaelezwa kuwa alishindwa kuyalipa.

Aidha inasemakana kuwa madeni hayo ni kutoka kwenye kikundi chake cha kikoba ambacho amejiunga na kujikuta amechukua mikopo mingi ambayo mwisho wa siku imemuelea na kukosa namna ya kuilipa na mwisho wa siku kuamua kujiua kwa kamba.

Kamanda Maigwa amesema tukio lilitokea juzi majira ya saa 1:00 usiku baada ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mashujaa, kutoa taarifa kituo cha polisi kuwa Milanzi amekutwa nyumbani kwake akiwa amejinyonga na kufariki dunia.

Aidha, madeni yamekuwa changamoto ya watu wengi ambapo kwa taratibu za mikopo kwenye vikundi mara nyingi endapo mtu ameshindwa kulipa madeni yake kikundi huamua kumfilisi kwa kuuza mali zake zenye thamani ya deni analodaiwa na wanachama.

Ni kweli dawa ya deni kulipa, lakini changamoto ni pale ambapo unakosa namna ya kuweza kulipa deni hilo.

 

Joel Matip amwaga wino Liverpool
Kaka mbaroni kwa kuhusika na mauaji ya mdogo wake