Serikali ya Awamu ya Tano imepanga kutoa ajira katika kada mbalimbali serikalini kwa kuajiri watumishi wapya 71,496 katika mwaka wa fedha ujao (2016/17), unaoanza Julai Mosi mwaka huu.

Mpango huo wa serikali umeelezwa Bungeni na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mbulu Mjini, Zacharia Issaay.

Waziri Kairuki alisema kuwa ingaewa serikali inakabiliwa na changamoto ya ufinyu wa bajeti, Serikali imeweka kwenye bajeti ijayo ajira mpya kwa idadi hiyo ya watumishi wakiwemo watendaji wa vijiji na kata. Alisema kuwa kwa watendaji wa Kata na Vijiji ajira zao zitaanza kutangazwa na kutolewa kuanzia mwezi ujao.

Alisema kuwa ajira za Serikali hutolewa kwa uwazi kwa kuanzia katika mchakato wa kuzitangaza na usaili unaofanyika.

Azam FC Vs JKT Ruvu Himid, Wanga Kurejea kikosini, Aggrey, Migi Nje
Messi Aleta Kizazaa Kwenye Familia Ya Mtoto Murtaza Ahmadi