DSCN3744

Miongoni mwa changamoto zinazo mkabili kijana wa Kitanzani ni Ajira ambapo kwa kuliona hilo makampuni mbalimbali ya kichina yamejitokeza katika maonesho ya ajira yanayoendelea katika viwanja vya michezo vya chuo kikuu cha dar es salaa huku wanafunzi wa Elimu ya juu wametakiwa kuwa wepesi katika uchangamikiaji wa fursa hizo.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Leornad Akwilapo wakati akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kufungua rasmi maonesho hayo, ambapo  jumla ya ajira zaidi ya mia tano zinatarajiwa kupatikana katika sekta mbalimbali za waekezaji hao kutoka china.

Kwa upande wake naibu makamu mkuu wa chuo tafiti na ubadilishanaji maarifa professor Cuthbert Kimambo amewahimiza vijana wa kitanzania kuichangamkia fursa hiyo kwa kujitokeza na cv zao zilizoandaliwa vyema na kujieleza vizuri kwani ushindani katika soko la ajira kwa hivi sasa ni mkubwa.

Ubalozi wa china uliwakilishwa na muambata wa kisisasa wa ubalozi huo, Zhang Biao ambaye amesisitiza nia thabiti ya china kuwekeza Tanzania huku akikumbushia kuwa undugu baina ya china na Tanzania ulianza miaka mingi.

DSCN3766

Maonesho hayo ya siku mbili yanatarajiwa kukamilika siku ya jumapili kwa awamu ya kwanza na yatakuwa yakifanyika mara kwa mara kutegemea na mahitaji ya wawekezaji hao wa kichina.

DSCN3770

Cleveland Cavaliers Mabingwa Wa NBA 2015-16
Video: Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani. CCM: Gwajima mchonganishi - Magazeti Juni 20 2016