Katika hali isiyo rahisi kuikubali kibinadamu, mwanume mmoja wa Urusi amejitolea kukatwa kichwa chake na kupandikiziwa mtu mwingine, katika oparesheni ya kwanza ya majaribio kwa binadamu.

Valery Spiridonov, mwenye umri wa miaka 31 ameruhusu jopo la madaktari 80 litakaloongozwa na Dkt. Xiaoping Ren kutoka China kufanya operesheni hiyo mwakani.

Operesheni hiyo ya kwanza kufanyika duniani inatarajiwa kugharimu kati ya Dola za Kimarekani milioni 10 hadi milioni 100.

Dkt. Xiaoping Ren amedaiwa kufanya operesheni kama hiyo iliyofanikiwa kwa wanyama kama panya na nyani. Madaktari hao wanadai kuwa wanaamini kwa wastani wa asilimia 90 kuwa upasuaji huo utafanikiwa kwa binadamu.

Valery Spiridonov anasumbuliwa na ugonjwa unaonyong’onyeza misuli unaofahamika kitaalam kama ‘Werdnig-Hoffmann’.

FA Wamtega Sergio Aguero
Werder Bremen Wapinga Kuzidiwa Kete Na FC Bayern Munich