Afisa wa zamani wa soka nchini Argentina amejiua baada ya kuhusishwa katika kashfa ya rushwa iliyotajwa na shirika la upelelezi la Marekani.

Jorge Delhon amejirusha kwenye reli na kukanyagwa na treni kwenye mji mkuu wa Argentina Buenos Aires ili kuweza kuepukana na tuhuma hizo za rushwa ambazo tayari zilikuwa zimeanza kufanyiwa kazi.

Aidha, Baadhi ya viongozi wa soka nchini Argentina wamesema kuwa wamesikitishwa na tukio hilo na kusema limetia doa kwenye soka la nchi yao kwani tukio hilo ni la kwanza kutokea katika historia ya nchi hiyo.

Hata hivyo, kesi ya Delhon iliyofunguliwa siku ya Jumatatu inafuatia upelelezi wa muda mrefu uliofanywa na Marekani kwenye shirikisho la soka duniani FIFA.

Kamati ya Bunge yawaweka kitimoto waandishi wa habari
Bob Chacha Wangwe ahukumiwa kwenda jela