Mtu mmoja nchini Afrika Kusini amekamatwa na kushtakiwa mahakamani mara baada ya kumtupa mtoto wake wa mwaka mmoja kutoka juu ya paa la nyumba yake.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 38 alichukuliwa katika kanda ya video akimrusha mtoto huyo wakati wa maandamano dhidi ya uvunjanji wa mitaa ya mabanda katika mji wa pwani wa Port Elizabeth.

Aidha, tukio hilo limetokea wakati polisi walipokuwa wakivunja vibanda 150 katika makaazi ya Joe Slovo ambayo wanasema yalijengwa kinyume cha sheria.

Hata hivyo, inasemekana kuwa mtu huyo alichukua hatua hiyo mara baada ya nyumba yake kutaka kuanza kuvunjwa na imeripotiwa kuwa alisaidiwa na mke wake kupanda juu ya paa hilo.

 

Aliyedai kuwa ni mtoto wa Lowassa atiwa mbaroni
Mvua zaendelea kuleta madhara nchini