Mwanaume mmoja nchini Marekani amekamatwa kwa kosa la kutoa uume wake hadharani kwenye duka moja kubwa la manunuzi na kuuweka kwenye mashine ya ukaguzi (checkout scanner) mithili ya bidhaa inayotaka kukaguliwa.

Haffingtton Post imeeleza kuwa kwa mujibu ulipata nyaraka za polisi kuhusu mkasa huo uliotokea Juni 22 mwaka huu. Ripoti hiyo ilieleza kuwa mwanaume huyo aliyetajwa kwa jina la Christian Fisher alifika katika duka hilo na kwenda mbele ya mashine hiyo iliyokuwa ikisimamiwa na binti mmoja na akafanya ‘wehu’ huo.

Imeeleza kuwa mshtuko uliooneshwa na binti huyo ulivuta usikivu wa mlinzi aliyekuwa akipita karibu. Mlinzi huyo alishuhudia tukio hilo. Fisher anadaiwa kutoshtushwa na lolote na alionekana akicheka.

Polisi walimshughulikia Fisher ambaye alionekana kutokuwa na tatizo la akili awali na amefunguliwa kesi ya kuweka hadharani nyeti na shambulizi la kudhuru mwili kwani alileta ‘matata’ katika eneo hilo baada ya kutaka kudhibitiwa na wana usalama.

Serikali yafafanua taarifa za ‘kupima ukimwi nyumba kwa nyumba’
Chris Brown adai atalaumiwa kwa kifo cha 2PAC, Suge Knight amshtaki