Jeshi la Polisi linatarajia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa wa mauaji’ Muhiri Nyankaira 35 mkazi wa kijiji cha Kiongera wilayani Tarime mkoani Mara kwa tuhuma za kumuua Baba yake wa ukoo Nyankaira Nyankaira Mrimi 65.
 
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake kamanda mkoa wa Kipolisi,Tarime/Rorya, Henry Mwaibambe amesema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 na dakika 5 Mei 17, 2019 katika shamba la mahindi.
 
“Mnamo Mei,17,2019 majira ya saa 3 na dakika 5 katika shamba la Nyankaira Nyankaira Mrimi lililopo katika kitongoji cha Robatende (A) kijiji cha Kiongera Nyankaira Nyankaira Mrimi 65 aliuawa kwa kuchomwa kwa kisu shingoni na kukatwa koromeo na mtoto wake Mhiri Nyankaira chanzo cha mauaji ni mgogoro wa Ardhi,“amesema Mwaibambe.
 
Aidha, Mwaibambe ameongeza kuwa marehemu alifungua shauri la madai ya ardhi namba 13/2019 katika Baraza la Ardhi la Kata ya Susuni kwa lengo la kubatilisha Umiliki wa Ardhi aliyoigawa kwa mtuhumiwa pamoja na Juma Nyankaira (33) kitendo ambacho mtuhumiwa hakukiafiki na kuahidi kufanya tukio kubwa pindi alipoitwa ndani ya Baraza la Ardhi la kata Tarehe7,5,2019 na kwamba hatarudi katika Baraza hilo tena.
 
Hata hivyo, Kamanda huyo ameitaka jamii na wakazi wote wa mkoa wa kipolisi, Tarime/ Rorya kuacha kujichukulia sheria mkiononi badala yake watumie njia ya sheria kuchukua mkondo wake.
Video: Maroroso Chadema, Lissu ataja rasmi tarehe ya kurudi
LIVE: Yanayojiri Bungeni jijini Dodoma Mei 23, 2019

Comments

comments