Mkazi wa kijiji cha Misisi Wilaya ya Mlele, Jilangu Seni (33) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na kipande cha jino la tembo ambacho thamani yake haijajulikana.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, ACP Ally Makame ameeleza kuwa mtuhumiwa amekamatwa na jino hilo akiwa amelihifadhi chumbani kwenye juu ya paa la nyumba.

 “Lilikuwa kwenye mfuko na alificha chumbani kwake juu ya dari,” amesema Kamanda Makame.

Aidha ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika jalada litafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

“Hili tatizo limepungua tunaendelea kupambana na hawa majangili, nitoe rai kwa wananchi wenye tabia hiyo waache mara moja wakibainika watawajibishwa kwa mujibu wa sheria,”

Kamanda Makame metoa angalizo kwa wananchi waliokaidi agizo la kusalimisha silaha wanazomiliki kinyume cha sheria kwa hiari akisema watasakwa.

Country Boy ajitoa Konde Gang
Akamatwa akipata chanjo ya Corona mara ya 11