‘Hitmaker’ wa Papa, Gift Stanford maarufu kama Gigy money ameahidi kumkomesha mfanyabiashara maarufu Afrika Mashariki, Zarinah Hassan kutokana na dharau alizomuonesha kupitia moja ya ‘post’ iliyokuwa ikisambaa mtandaoni.

Gigy ameapia katika nafsi yake kuwa katika maisha yake atahakikisha anazaa na mtoto wa kwanza wa kiume wa Zari ili aweze kuheshimika na Zari kama binti yake lakini pia kama mkwe wake.

Gigy amewaza kufanya hayo ili aweze luheshimika na Zari ambaye amemwonesha dharau waziwazi anaamini kwa kufanya hivyo itamfanya Zari aweze kujishusha kwake.

”Sasa Zari mimi nakuahidi kuwa lazima nizae na mwanao wa kwanza ili wewe uwe bibi wa mwanangu, ndio ataniheshimu halafu yeye atakuwa mama mkwe wangu na hatokaa aamini  nitakapopita na mwanae wa kwanza na kuzaa nae.

Gigy Money amekuwa akisema kuwa mwanamama Zari amekuwa na dharau sana hasa kwa watanzania na kuwa amekuwa akiwajibu vibaya kutokana na hali yake ya kujiita ‘bossy lady’.

Mbali na hayo hivi karibuni Gigy Money ameingia kwenye ugomvi mzito na Zari mara baada ya Zari kuandika mtandaoni kuwa asifananishwe na Gigy, hali ambayo Gigy ilimfanya ajione amedharaulika na kuhoji asifananishwe naye kwa ni yeye amekuwa mnyama.

Hivyo Gigy nae kujitoa unyonge amekuwa akitoa kauli mbalimbali juu ya Zari kuonesha kwamba hata yeye yupo juu na ipo siku atakuwa na fedha zaidi ya alizonazo Zari na kumtaka Zari aache kudharau binadamu wenzie.

 

Walimu 4 mbaroni kwa wizi wa mitihani darasa la 7
Simon Mignolet aenguliwa kambi ya Ubelgiji

Comments

comments